MAJIBU YA HOSPITALI YENYE UTATA YA MUHATARISHA MAISHA MARYAM.

Na Tatu Juma Zanzibar,

Kijana Maryam Ali Mussa mwenye umri wa miaka 32 Mkaazi wa Magomeni Jitini Mkoa wa Mjini Magharib Unguja amekubwa na taharuki baada ya kupata majibu kutoka Spitali ya Occupation health Unity na hatimae kupoteza fahamu na kujenga wasiwasi mkubwa kwa familia yake.

Maryam ambae ni mjasiri amali wa biashara ndogo ndogo ameeleza kuwa taharuki hiyo ilimtokezea baada kupima vipimo stahiki kwa kila mfanya biashara katika hospitali hiyo iliyopo Migombani Mjini Magharib Unguja na hatimae kupata majibu asiyoyatarajia ambayo ni (POSITIVE)

Amesema kuwa baada ya kupima vipimo vyote aliruhusiwa kurudi nyumbani sikuyapili yake alitafuta ufumbuzi wa majibu hayo na kuambiwa yapo positive kitendo ambacho kilimsababisha kupoteza fahamu.

“Wakati nataka kufungua biashara nia yangu ni kuuza supu nilifuata njia za kisheria kwakuanza kwenda manispaa baada ya hapo nikambiwa niende hospitali ya Covid nikapime vipimo vyote lakini majibu wakanambia watanitumia kwenye simu,majibu yaliporushwa nikayatoa nakutafuta utambuzi lakini nikaambiwa nipo positive kwamaana nina ugonjwa fulani kitendo ambacho kiliniishia nguvu na kuanguka chini”

“Baada ya hapo nikapelekwa spital ya magereza nikapata matibabu baadae nikazindukana na kuambiwa sina magonjwa yoyote ispokua cheti cha cofid kinasema ninatatizo la Typhod wakanipima tatizo la Typhoid pia ikaonyesha sina tatizo ilo”amesema maryam

Nae mama mzazi wa kijana huyo Amana Suleiman Mzee ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ kufanya uchunguzi wa kina spitali zote mbili ili wananchi waondokane na simtofahamu kama hizo.

“Manaake wanatutia taharuki,wajasiriamali, wanyonge unakwenda kupima elfu hamsini na tatu, unakwenda kupima tena elfu kumi na tano,tunakuomba Rais wetu ichunguzwe spitali ya Magereza au iyo ya covid” amesema Bi Amana Suleiman

Akizungumza na waandishi wa habari vyombo tofauti Afisa wa kitengo cha upimaji wa afya za wafanyakazi, Zainab Abubakar amesema kuwa maranyingi inajitokeza changamoto ya watu kupimwa tyfod na kugundulika wanatatizo hilo lakini maranyingi watu hao wanakwenda spitali nyengine nakuambiwa hawana.

“Imeshatokea kwamba mtu hajaamini majibu,anaenda spitali nyengine anakwambia sina Typhoid imesoma negative tumeshalifatilia ilo swala tulivyokuja kuangalia lile chimbuko nikwamba hawapewi majibu ya uhakika anamwambia daktari amuwekee kwamakusudi negative”amesema Afisa Zainab

Kwa mujibu wa baadhi ya wafanya biashara wanaokwenda kupima vipimo kitengo hicho wamebaini kuwa wengi wao wanathibitika kuwa na tatizo la Typhoid.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *