MKURUGENZI AKABIDHI BASKELI 30 KWA WANAFUNZI WA ELIMU MBADALA KASKAZINI A.

Na Tatu Juma Zanzibar

Mkurugenzi wa Elimu Mbadala na elimu ya watu wazima Mashavu Ahmad Fakih amewakabidhi Baskeli 30 kwa wanafunzi wa darasa maalumu ili kurahisisha usafiri wakati wanapokwenda kujiendeleza kimasomo huko Afisi ya Elimu Wilaya ya Kaskazini ‘A’

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada tu yakumalizika hafla hiyo amesema miongoni mwa mikakati ya Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania na Zanzibar ni kuisaidia jamii kielimu hivyo kwa sasa imeamua kuwapa elimu watoto pamoja na vijana waliokata masomo kwa kuwapa ujuzi mbali mbali ili kuweza kujikwamua kimaisha.

Amesema lengo kuu la msaada huo ni kuwawezesha kupata urahisi wa usafiri ili wapate urahisi wa kuweza kupata taaluma ya kujua kusoma na kuandika, kujua hesabu,pamoja na masuala mbali mbali ya ujasiriamali.

“Tunamikakati mingi yakuwasaidia vijana ambao wapo nje ya uwepo wa skuli,tunaamini ujuzi hauzeeki,kwamfano hapa mkwajuni tunawapa ujuzi wa kuendesha bodaboda,tunao boda boda hawa wanawake,tunawajasiriamali wa kutengeneza sabuni,tunao wachongaji,tunao mafundi umeme,mambo yautunzaji nyumba na udobi,tunazo fani nyingi kwaajili ya kuwasaidia vijana”.amesema Mkurugenzi

Nae Afsa Elimu Wilaya Kaskazini ‘A’ ndugu Juma Mwadini Abdallah amesema ingawa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Wizara ya elimu na mafunzo ya Amali inajitahidi kutoa muamko lakini Wilaya hiyo ipo katika mazingira ya utalii na baadhi ya vijiji bado wazazi hawana muamko kwa watoto wao juu kuwafichua na kuweza kupata elimu.

Amesema kuwa kwasasa wamefanikiwa kwakiasi kikubwa kupitia programu mbalimbali kwa kuzunguka ndani ya shehia tofauti Wilayani humo na hatimaye kuwaibua vijana walioacha masomo na sasa wameweza kupata masomo na mafunzo madhubuti.

“Kwa Wilaya ya Kaskazini A wapo hasa ukanda wa pwani,kama vile kijini, kuna shehia kama yakidombo,mkwajuni hapa kidogo lakini hasa shehia zile za ukanda wa pwani pembeni mbembeni au kuna sehemu inaitwa kidagoni kuna asilimia sana ya vijana hawa hususan watoto wa kike wameacha masomo”amesema Afsa Juma

Kwaupande wake mwanafunzi aliyejiunga na elimu hiyo Jamila Omar Muhammed mkaazi wa Chaani Juwakuu amesema kuwa amepata manufaa makubwa baada ya kujiunga na darasa hilo kwani kwasasa anauwezo wakusoma nakuandika kwa ufasaha zaidi pamoja na kupata ujuzi wa masuala ya ujasiri amali.

Amesema kutokana na elimu anayoipata darasani hapo matarajio yake ya baadae nikujiajiri na hatimaye kuweza kupata kipato chake cha halali.

Mradi huu unaotambulika kwa jina la Daraja umeshirikisha tume ya Taifa Tanzania bara uliolenga maeneo matatu ikiwemo Masasi,Geita na Zanzibar ambapo kwa hapa Unguja umeanzia Kaskazini A Unguja ambao unalengo la kuinua jamii kielimu na kimaisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *