PROf.MKENDA AZINDUA DURU YA NNE TUZO YA UANDISHI UBUNIFU

DAR ES SALAAM : DURU ya nne ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu kwa mwaka 2025/2026 imezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam, huku waandishi wa habari wakihimizwa kujiandaa na kuwasilisha miswada yao kwa ajili ya kushiriki katika mchakato wa ushindani.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa huu ni wakati muafaka kwa waandishi wa habari kuwasilisha kazi zao za ubunifu kwa Kamati ya Kitaifa ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, kwa lengo la kuendeleza jitihada za kukuza uandishi na matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini.

“Tuzo hii ni sehemu ya dhamira ya serikali kuendeleza urithi wa fikra na maono ya Mwalimu Nyerere kupitia lugha ya Kiswahili na uandishi wa ubunifu. Tunawakaribisha waandishi wote kushiriki kwa wingi,” alisema Prof. Mkenda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *