WAISLAMU WATAKIWA KUJITOLEA KUMALIZIA UJENZI WA MASJID SUNNAAH MUWANGE

Na Abdulkadir  Sakaza

Akiripoti kutoka Muwange, Zanzibar

Ujenzi wa misikiti ni mojawapo ya njia muhimu za kuendeleza mshikamano wa kijamii, ibada za pamoja, na malezi ya dini katika jamii ya Kiislamu. Kijiji cha Muwange, kilicho kaskazini mwa Unguja, kimeonyesha mfano wa mshikamano huu kupitia ujenzi wa Masjid Sunnaah, ambao umeanza mwaka 2016 na unaendelea kwa jitihada za wanajamii, wahisani, na wafadhili mbali mbali.

Akiufungua rasmi msikiti huo wa Masjid Sunnaah , Sheikh Musa Juma amesema jitihada za wanajamii kujitolea si tu ni sehemu ya ibada, bali pia ni fursa ya kudumisha mshikamano wa kijamii na kueneza maadili ya Kiislamu. “Ujenzi wa msikiti ni fursa ya kutoa mchango wetu kwa Mwenyezi Mungu, na ni mfano wa mshikamano wa kijamii unaoonyesha jinsi jamii inavyoweza kushirikiana,” amesema Sheikh Musa.

Naye Sheha wa Shehia ya Muwange, Mcha Iddi Haji, amewaasa wanajamii kujitolea kikamilifu, wakitumia fursa hii kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuchangia ujezi wa msikiti. “Kila mmoja ana nafasi ya kuchangia, si kwa ajili ya mali tu, bali pia kwa sababu ya dhahiri ya ibada na mshikamano wa kijamii,” amesema Mcha Iddi.

Baadhi ya wanajamii wamesema kuwa kujitolea katika ujenzi wa msikiti ni sehemu ya maisha yao ya Kiislamu, hatua inayowaunganisha kijamii na kiroho. Bi Aisha Saleh, mkazi wa Muwange, anasema: “Tunajitolea kwa furaha ili kuona msikiti ukikamilika na kuwa kituo cha ibada na malezi ya dini.”

jumla ya Shilingi milioni 35.5 zimekwishatumika, huku gharama zilizobaki ni Shilingi milioni 25, Hii inamaanisha bado kuna hitaji la michango zaidi kutoka kwa wanajamii, wahisani na wafadhili ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati huku Vifaa vinavyohitajika kumalizia msikiti hui ni, Kokoto, Jipsam Bodi, Jipsam Poda, Taizi, Rangi Na Milango Na Nondo, Saruji, Bati na Mchanga.

Masjid Sunnaah Muwange ulianza kujengwa mwaka 2016, ukiwa na lengo la kuhudumia idadi kubwa ya waumini wa muwange na maeneo Jirani ambao Baada ya kukamilika, msikiti utakuwa na uwezo wa kubeba waumini 600.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *