TANZANIA KUKUMBWA NA MVUA KUBWA YA SIKU 3 KUANZIA LEO

Tanzania inatarajia kupata mvua kubwa zitakazodumu kwa kipindi cha siku tatu kwenye ukanda wake wa Pwani, kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo (TMA). Taarifa ya mvuo hizo iliyochapichwa na Mwanananchi mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia tarehe 26 hadi 28 Oktoba.

Mikoa iliyoainishwa kukumbwa na hatari ya mvua kubwa ni Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa hiyo inasema mvua hizo zinaweza kuambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa pwani, kutokana na msukumo wa kimbunga kinachoitwa Tropical Storm Chenge kinachozidi kusogea Magharibi mwa Bahari ya Hindi.

Mamlaka hiyo ya Hali ya Hewa inasema inaendelea kufuatilia maendeleo ya kimbunga na mvua hizo.

Hata hivyo, baadhi ya wataalam wa hali ya hewa wanasema kuwa kiwango cha mvua kinategemea mabadiliko ya haraka ya mfumo wa hali ya hewa, na kuhimiza wananchi kufuatilia taarifa rasmi mara kwa mara kupitia vyombo vya habari na tovuti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuchukua tahadhari.

Chanzo:BBC Swahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *