Mahakama ya Korea Kusini imemhukumu kifungo cha maisha jela mwalimu mmoja kwa kumdunga kisu mtoto wa miaka minane, katika kesi iliyoshtua taifa hilo.
Myeong Jae-wan, 48, alimuua Kim Hae-neul, baada ya kumshawishi kuingia darasani katika mji wa kati wa Daejeon mwezi Februari.
Waendesha mashtaka walikuwa wameomba hukumu ya kifo kwa Myeong, wakisema kuwa familia ya mwathiriwa iliomba adhabu kali.Lakini mahakama ilisema ingawa “hatari ya kudhulumiwa tena ni kubwa, ni vigumu kuhitimisha” kwamba Myeong lazima auawe.
Myeong alisema kwamba atatafakari makosa yake katika maisha yake yote.Alisema uwezo wake wa kufanya maamuzi haukuwa sawa wakati wa kisa hicho alipokuwa akipokea matibabu ya afya ya akili.
