Na mwandishi wetu
Akiripoti kutoka Chakechake Pemba
Wadau wa utekelezaji wa mradi wa uhimilivu wa mabadiliko ya tabia ya nchi Zanzibar wametakiwa kusimamia, kuhifadhi na kulinda mazingira katika maeneo yao ili kuzuwia athari za mabadiliko ya Tabianchi zisiendelee katika jamii.
Akizungumza katika kikao cha mradi huo Mkurugenzi uratibu tawala za Mikoa Serikali za Mitaa Zanzibar Zainab Khamis Kibwana wakati akifungua kikao cha kuutambulisha mradi huo kwa Mamlaka za serikali za Mitaa kwa upande wa Pemba kilichofanyika katika ukumbi wa Baraza la Manispaa Chake chake Mkoa wa kusini Pemba.

Amesema Mradi wa uhimilivu wa madaliko ya Tabia nchi (Scale Program) utasaidia kurejesha maeneo ambayo tayari yameathirika na mabadiliko hayo na kuyarejesha katika hali yake ya kawaida na kuyalinda maeneo mengine ili athari hizo zisiweze kujitokeza kwenye jamii.
Akiwasilisha mada katika kikao hicho mratib wa mradi kutoka Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Jaku Abdalla Jaku amesema utekelezaji wa mradi huo utahusisha wananchi katika uibuaji wa fursa, na kuwataka watendaji kutumia fursa hiyo kwa kushirikiana na wanachi kuibua miradi itakayowawezesha kukukuza maendeleo katika Nyanja mbali mbali.

Nao wadau wa utekelezaji wa mradi huo kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa wamesema mradi huo umekuja wakati muafaka kwani yapo maeneo mengi ambayo tayari yameathirika hivyo wameshukuru kwa kuja mradi huo kwani utawasidia wananchi kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi sambamba na kukuza hali zao za kiuchumi.
Mradi huo wa Miaka mitano unadhaminiwa na Benki ya Dunia Ambapo unatekelezwa katika ngazi ya jamii kupitia Manispaa 64 nchini ikiwemo Halmashauri zote11 za Zanzibar.
