MASHINDANO YA SQUASH AFRIKA KUFANYIKA ZANZIBAR MWAKANI

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab ameahidi kushirikiana na Shirikisho la Mchezo wa Ukuta (SQUASH) Afrika ili kuleta maendeleo ya Michezo hususan Mchezo huo.

Ameyasema hayo wakati Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Ukuta Afrika (SQUASH) Dr. Lucky Mlilo alimtembelea Ofisini kwake Migombani Wilaya ya Mjini.

Aidha Katibu Fatma, amepokea kwa mikono miwili ombi la Raisi huyo, kuandaa mashindano Squash kwa Watu wenye umri wa miaka 35-85 (Masters) ambayo hayajawahi kufanyika Nchi yoyote Barani Afrika na mara ya kwanza, yanatarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar.

Hata hivyo amesema katika viwanja vitakavyojengwa Wizara katika Mji wa Michezo Fumba, itahakikisha inajumuisha Viwanja vya Mchezo wa Ukuta (Squash).

Kwa upande wake Kamishna Idara ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ameir Mohammed Makame amesema, mashindano hayo, yataweza kutoa fursa kwa Wachezaji, kuongeza Mapato kwa Serikali na Wageni kutembelea sehemu mbalimbali.

Nae Rais wa Dk. Lucky Mlilo amesema lengo la kuja Tanzania ni kutoa mafunzo kwa Wachezaji na Waamuzi wa Mchezo huo ambayo Tanzania bara yamefanyika wiki iliopita na upande wa Zanzibar yamefanyika leo.

Hata hivyo Rais huyo, ameiomba Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuboresha na kuweka mikakati inayokubalika kitaifa, kikanda na kimataifa ya mchezo huo ili kupata fursa ya kuandaa mashindano mbalimbali ya Mchezo huo.

Ziara ya Rais wa Mchezo wa Squash Afrika Dr. imefanyika Nchini kwa lengo la kuangalia Changamoto wanazokabiliana nazo ili kuweza kuandaa mashindano ya kimataifa, yanatarajiwa yanatarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar hapo mwakani.

Imetolewa na kitengo cha Habari, WHVUM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *