JAMIII ACHENI MILA NA DESTURI ZENYE MADHARA

Na Mariam Matundu.
Serikali inaendelea na juhudi za za kutoa elimu kuhusu masuala ya mila na desturi zinazofaa na zile zisizofaa kuwepo kwenye jamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

Hayo ymeelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Neema Ndoboka wakati akifungua kikao cha wadau wanaotekeleza eneo la mila na desturi katika Mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili zidi ya Wanawake na Watoto (MTAKKUWA) kilichofanyika leo (tarehe17, 2025) jijini Dodoma.

Bi Neema amewaasa wadau wa maendeleo kuongeza juhudi zaidi katika kupiga vita mila zenye madhara huku akisema kuwa wadau kamwen hawapaswi kutokukata tamaa kwa kuwa suala la jamii kukubali kuachana mila walizorithishwa wazee wao waliotangulia si jambo jepesi.

kwa upande wake Mratibu wa MTAKUWWA kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Alex Shayo amesema mpaka sasa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinaendelea kupungua baada ya jamii kupata elimu na kuhusiana na madhara ya mila na desturi zisizofaa

Nao wadau wa maendeleo wanaotekeleza afua hiyo wameishukuru Serikali kwa ushirikiano wake katika kutokomeza mila na desturi potofu na kuahidi kuendelea kupambana ili kuleta fikra chanya na jamii inayojitambua kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *