Na Rahma Khamis
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria ,Utumishi na Utawala Bora Dr Haroun Ali Suleiman amewapongeza watendaji wake kwa ushirikiano wao katika kipindi chote Cha miaka mitano Cha utendaji wake.
Pongezi hizo amezitoa huko Ofisini kwake baada ya kupokea taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa Ofisi hiyo kwa kipindi Cha miaka mitano.
Amesema kuwa mafanikio hayo yanatokana na maono ya Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi katika kuibadilisha Zanzibar kimaendeleo.
Aidha amewaasa watumishi hao kuendelea kudumisha Amani na Utulivu iliyopo nchini ili kufanikisha Uchaguzi Mkuu unayotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Akitoa taarifa ya mafanikio hayo Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Omar Haji Gora amesema kuwa Ofisi imefanikiwa kuratibu Miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo ikiwemo upatikanaji wa haki na Tanzania Feature.
Amesema kuwa katika kuimarisha jamii Ofisi imefanikiwa kutoa huduma ya Msaada kisheria kupitia Kampeni ya Mama Samia kwa wananchi lakini nne sitini na mbili Elfu mia Tisa na nane kwa wanawake na wanaume.
Ameongeza kuwa Ofisi imefanikiwa kuimarisha maslahi ya watumishi wa Umma kwa kufanya marekebisho,kulipa posho la nauli kwa wafanya kazi sambamba na posho la Wakuu wa Divisheni kwa Wizara zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ameeleza kuwa Ofisi imeimarisha mifumo ya kieletroniki ya Utoaji wa huduma za jamii ikiwemo Zanajira pamoja na watumishi 14 kupatiwa mafunzo nchini Japan

Akitoa neno la shukrani Naibu Katibu Mkuu Katiba na Sheria (OR KUSSB) Mzee Ali Haji amesema kuwa Ofisi hiyo imesimamia Taasisi zake kwa ubora wa hali ya juu.
Aidha amefahamisha kuwa wataendelea kujifunza kutoka kwa Kiongozi huyo ili kuweza kufanya vyema zaidi kwani mafanikio hayo yanatokana na uimara na weledi wa utendaji wake.
