UNGUJA UKUU WAITAKA SERIKALI KUIFUNGIA BAA INAYOWAFUNDISHA WATOTO WAO NGONO

Na Abdul Sakaza

Wananchi wa Shehia ya Unguja Ukuu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, wameibua malalamiko mazito dhidi ya baa moja inayojulikana kwa jina la KBN RESTAR wakiituhumu kuwafundisha watoto wao wadogo kufanya ngono.

Wameeleza kua jambo hilo halikubaliki katika kijiji Chao kwani linaenda kinyume na maadili ya jamii yao na taifa kwa ujumla, Kwamujibu wa Taarifa za wananchi hao zinaeleza kuwa baadhi ya watoto wamekuwa wakilazimika kwenda kupaa samaki maeneo ya pwani au kuiba nazi mashambani ili kupata fedha za kulipia gharama za huduma hizo ikiwemo kufundishwa vitendo hivyo vya ngono kwenye baa hiyo.

Baadhi ya wanawake wa kijiji hicho wanasema tatizo hili limekuwa sugu, na linahusisha pia kuvunjika kwa ndoa kwani waume zao ni miongoni mwa wanaofata huduma hizo katika baa hiyo hali ambayao inavunja kabisa misingi ya ndoa na familia.

“Hii si mara ya kwanza tunalalamika Tumeshawahi kutoa taarifa kwa viongozi wa shehia, lakini tunataka sasa hatua za wazi zichukuliwe ,Maadili ya jamii yetu yanashuka na hii baa inachangia pakubwa.” alisema mwananchi mmoja

Sheha wa Shehia ya Unguja Ukuu, Khamis Ibrahim Shomari amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na amesema ofisi yake imepokea malalamiko hayo mara kadhaa na tayari uongozi wa shehia umechukua hatua mbali mbali ikiwemo kuzifikisha taarifa hizo kwa viongozi wa juu .

Kwa upande wake, mmiliki wa baa ya Kae Bona, Ali Musa, amepinga tuhuma hizo akizitaja kuwa ni za uongo na zenye nia ya kuichafua biashara yake kwani katika baa hiyo hakuna vitendo viovu vinavyofanywa ikiwemo kuwafundisha watoto wadogo kufanya ngono

“Hii ni biashara halali, inayoendeshwa kwa mujibu wa taratibu zote za kisheria. Hapa tunauza vinywaji tu na Sijawahi na sitawahi kuruhusu vitendo vya aina hiyo” alisema mmiliki wa baa hiyo

Mkuu wa Wilaya ya Kati, Rajab Ali Rajab, amesema serikali ya wilaya itachunguza kwa kina tuhuma hizo na zikibainika zinaukweli wataifungia baa hiyo kwani suala la kuharibu maadili ya jamii ni jambo lisilovumilika hata kidogo na kuwataka wananchi wa unguja ukuu kua na subra katika kipindi hichi kwani jambo hilo linafatiliwa na kupatiwa suluhu ya kudumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *