WATU WENYE ULEMAVU 8,021 KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU OKTOBA, JE WANAMAONI GANI?

Jumla ya watu wenye ulemavu wapatao 8,021 wanatarajiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa oktoba mwaka 2025 visiwani Zanzibar.

Taarifa hii imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), ambaye ameeleza kuwa idadi hiyo inatokana na takwimu rasmi zilizokusanywa kupitia mchakato wa uandikishaji wa wapiga kura.

Ushiriki wa kundi hili ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakuwa jumuishi na shirikishi, unaoheshimu haki za kiraia na kisiasa za watu wote bila ubaguzi.

Aidha, ZEC imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha mazingira rafiki na miundombinu wezeshi katika vituo vya kupigia kura, ili kuwapa fursa sawa watu wenye ulemavu kushiriki ipasavyo.

Hii ni pamoja na hatua za kiufundi na kisheria zinazolenga kuondoa vikwazo vinavyoweza kuathiri ushiriki wao, na hivyo kuimarisha demokrasia na usawa katika Zanzibar.

Nilizungumza na watu wenye ulemavu mkoa wa kaskazini unguja wamesema wameridhishwa na hatua za ZEC,Mmoja wa wapiga kura wenye ulemavu wa kuona, Asha Suleiman, alisema Ni jambo la faraja kuona kwamba tumepewa fursa ya kushiriki uchaguzi kwa usawa”Miundombinu ya vituo vimeboreshwa, na hivyo kuondoa hofu ya kushindwa kupiga kura.” alisema

Mwingine, Ali Juma, mwenye ulemavu wa viungo ameweka bayana kua “Habari hizi zinatupa motisha. Hii inaonyesha kwamba haki zetu za kiraia zinaheshimiwa, na tuna nafasi ya kuchangia katika uchaguzi bila vizuizi.” alisema kwa matumaini

Hivyo, hatua za ZEC zimepokelewa kwa shukrani na matumaini na watu wenye ulemavu, ambao wanatarajia kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa oktoba mwaka 2025.

One thought on “WATU WENYE ULEMAVU 8,021 KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU OKTOBA, JE WANAMAONI GANI?

Leave a Reply to Siti Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *