Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza kwa masikitiko kifo cha Mbunge wa Jimbo la Isimani na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Vangimembe Lukuvi, kilichotokea leo Machi 25, 2026, majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, alipokuwa akipatiwa matibabu kufuatia mshtuko wa moyo.
Taarifa ya msiba huo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, na kuthibitishwa kwa kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusiluka.
Marehemu Lukuvi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Isimani mkoani Iringa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akisimamia sera, uratibu wa shughuli za Serikali pamoja na masuala ya watu wenye ulemavu.

Lukuvi ambaye alizaliwa Agosti 15, 1955, alikuwa Bungeni kwa kipindi cha Saba ikiwa ni tangu Mwaka 1995 ulipofanyika Uchaguzi wa Mfumo wa Vyama Vingi nchini.
