WANAWAKE PIGENI KURA KUTIMIZA WAJIBU WENU

NA FAUZIA MUSSA

WANAWAKE wenye sifa wamehimizwa kushiriki uchaguzi ifikapo oktoba 29 kupata haki yao ya kupiga kura na kusisitizwa wajibu wao wa kutunza amani iliyopo nchini.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya kuwawezesha Wanawake kiuchumi na haki za binaadamu (ZAWEHA), Thneyyu Mabrouk Hassan baada ya dua ya kuiombea nchi na viongozi wake ilioandaliwa na Jumuiya hiyo kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

Thneyyu aliwaomba akina mama hao Katika kipindi hiki na baada ya uchaguzi mkuu kuisha kuendelea kusimamia suala la amani kwani inapotea kundi kubwa linaloathirika ni wanawake, watoto, wazee na wenye ulemavu.” Tuzungumze na waume zetu na vijana wetu wa kiume vurugu zinapokuja wote wanaweza kujihami changamoto inabaki kwetu na watoto wetu” alisema Thneyyu

Pamoja na dua ya kuliombea taifa kuingia katika uchaguzi kwa amani alifahamisha kuwa mkusanyiko huo umelenga kuwakumbusha akina mama kushiriki kupiga kura na kuchagua viongozi wenye maono ya kutatua changamoto za kundi hilo na kuimarisha ustawi wao.”Itakapofika tarehe 29 oktoba mwaka usiwache kwenda kupiga kupiga kura kwani hiyo ni haki ya kila mwenye sifa bila kujali jinsia” alisema Thneyyu

Kwa upande wake mwanasheria wa ZAWEHA Miza Nahoda Juma, aliwakumbusha akinama hao kuwa jukumu la kutunza amani ni la kila mtu na sio tu kipindi cha uchaguzi bali katika siku zote za maisha yao.” Unaposhiriki kupata haki yako ya kupiga kura usisahau wajibu wako katika kusimamia na kutunza amani. Uchaguzi ni wa siku moja tu kila baada ya miaka mitano lakini amani ni tunu inayopaswa kutunzwa na kuwepo siku zote, piga kura rudi nyumbani ukasubiri atangazwe kiongozi aliechaguliwa na wananchi wengi na tusherehekee ushindi Kwa salama na amani bila kushajihishana vurugu litakaloathiri vizazi vyetu” aliwanasihi

Alieleza kuwa maendeleo wanayoyashuhudia na hata wageni wanaotutembelea kutoka Nchi mbalimbali ni kwasababu ya amani iliopo na endapo itakosekana mambo mengi hayatatekelezeka.

akizungumzia kuhusu Jumuiya hiyo Katibu wa ZAWEHA Zaina Mahmoud Salum alieleza kuwa ipo kwaajili ya kuhakikisha mwanamke anyanyuka na kushiriki katika nyanja zote ikiwemo za kisiasa, kijamii na kiuchumi pamoja na kuhakikisha kundi hilo linapata haki zao za kibinaadamu bila kujali rangi kabila wala chama na kuwakaribisha wanawake wote katika Jumuiya hiyo kupata fursa zinazotolewa.”Tunajua wanawake tunakabiliwa na migogoro mbalimbali ya familia, itumieni jumuiya hii kupata ushauri nasahi na pia kupata mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali ili kujiinua kiuchumi na kuepuka utegemezi wa asilimia 100.” Alisema

WAshiriki wa hafla hiyo waliishukuru ZAWEHA kwa kujitolea kuwahamsisha kushiriki uchaguzi kwa amani na kuahidi kuwa mabalozi wazuri ndani ya jamii zao.

Asha Amour Bakar alieleza kuwa uzoefu unaonesha kuwa wanawake ndio waathirika zaidi wa majanga yote yanayotokea duniani hivyo aliwaomba wanawake wenziwe Kuhamasishana kuitunza Amani.

Aliwashauri kuwasisitiza Vijana kutokufuata mihemko na badala yake kuendelea kusikiliza maelekezo ya viongozi wa nchi kuhusu mchakato wote wa kupiga kura kwa misingi ya amani Ili Taifa liendelee kuwa salama kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *