REUBEN SAGAYIKA AWEKA WAZI SERA ZAKE KWA WANANCHI WA MSUFINI KATA YA KALANGALALA

Na Ester Mabula

Mgombea udiwani wa kata ya Kalangalala kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Reuben Sagayika leo Oktoba 06, 2025 ameendeleza kampeni za kunadi sera zake na ilani ya CCM ambapo amezungumza na wakazi wa eneo la Msufini kata ya Kalangalala, halmashauri ya manispaa ya Geita.

Katika mkutano huo Sagayika amewaomba wakazi wa kata ya Kalangalala na wananchi kwa ujumla kuchagua viongozi watokanao na CCM katika ngazi za Udiwani, Ubunge na Urais ili kuleta maendeleo kwa Jamii.

Akizungumza mbele ya Mgombea Ubunge wa jimbo la Geita mjini Mhandisi Chacha Wambura ameyataja maombi matatu atakayoanza nayo baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo kuwa ni pamoja na mambo yanayohusu makundi ya vijana, wanawake pamoja na wazee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *