RAIS WA MADAGASCAR AOMBA MWAKA MMOJA KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI AKISHINDWA ATAJIUZULU

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ameomba muda wa mwaka mmoja kurekebisha changamoto za nchi hiyo, na kuahidi kuwa iwapo zitaendelea, atajiuzulu.

Alisema hayo wakati wa mkutano katika ikulu yake na makundi mbalimbali ya wafuasi wa serikali.

Wahudhuriaji wengi walipata fursa ya kumuuliza rais maswali au kuchangia maoni yao tu, ambapo alijibu.“Sitaki kubembeleza nataka kusikia ukweli, ni watu waliokuwa wakiniambia kila kitu kiko sawa ndio wanahusika na hali yetu ya sasa,” alisema.

Vuguvugu la maandamano hayo, linalojulikana kama Gen Z Mada limekuwa likitoa wito kwa rais kujiuzulu na kukataa mwaliko wa kuhudhuria mazungumzo hayo.

Wanasema kuwa hawawezi kushirikisha serikali ambayo imekuwa ikiwakandamiza kwani wanadai haki za msingi za binadamu,Kundi hilo limeitisha maandamano mapya siku ya Alhamisi. “Tunakataa mwaliko wa rais kwenye mazungumzo.

Hatutashiriki mazungumzo na utawala unaokandamiza, kuwashambulia na kuwadhalilisha vijana wake mitaani,” waliandika kwenye ukurasa wao wa Facebook.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *