MAHUJAJI 2,600 KUTOKA ZANZIBAR WANATARAJIWA KUHIJI MAKKA MWAKA 2026

Taasisi zilizo chini ya umoja wa wasafirishaji wa mahuajj Zanzibar (UTAHIZA) zimesema zitaendelea kutoa elimu ya ibada ya hijja kwenye mikushanyiko ya vijana ili kutoa hamasa kwa vijana hao kujitokeza kushiriki ibada ya hijja wakiwa mumri mdogo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kikao cha kuelezea maandalizi ya hijja na mwelekeo wake kwa mwaka 2026 kilichofanyika katika ukumbi wa Masjidi Jamiu Zinjibar Mazizini mjini Unguja katibu mtendaji wa wakfu na mali ya Amana Zanzibar Shekh Abdala Talibu amesema kuna haja ya kufikisha elimu ya hijja kwenye makundi ya vijana ili na wao waweze kufikiwa na fursa hiyo na kuitumia.

Amesema uzowefu unaonyesha watu wengi wanaohamasika na kushiriki kutekeleza ibada ya hijja ni wazee na ambao hupoteza sifa ya kutokuwa na Afya imara itakayowawezesha kumudu matendo yote ya hijja.Amesema kazi ya kwanza itakayofanywa na taasisi hizo ni kuondoa dhana potofu iliyojengeka kwenye jamii ya kuwa ibada hiyo ipo kwa ajili ya wazee na waatu wazima ambao hawana matumaini ya kuendelea na maisha baaada ya kurudi makka.

Katika hatua nyengine kiongozi huyo amewataka wale wote waliojisajili na kukubaliwa kushiriki ibada ya hijja mwaka huu kukamilisha malipo kabla ya mwezi march mwaka 2026 ili kuondokana na changamoto zinazoweza kujitokeza ikiwemo majina yao kuondolewa kwenye orodha ya mahujaji.

Akichangia maada katika mkutano huo Ndugu Mohamed Sulaiman kutoka taasisi ya Ahalu suna waljamaa ameomba uongozi wa UTAHIZA kuzifanyia kazi changamoto zinazojitokeza kwenye taasisi za hijja ikiwemo swala la kuongezeka kwa gharama za hijja mara kwa mara ili kuweka mazingira bora kwa mahujajji.

Jumla ya mahujaji wanaotarajiwa kutekeleza ibada ya hija kwa mwaka 2026 ni 4,000 ambapo mahujaji ni 2,600 kutoka mikoa ya Zanzibar na 1,400 mikoa ya Tanzania bara

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *