Na Juma Haji,
Jumuiya ya muangaza zanzibar imesema jamii inapaswa kujiepusha na mambo yanayoshajihisha uwepo wa viashiria vya uvujifu wa amani katika kipindi hiki cha campeni za kuwanadi wagombea kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025.
Akizugumza kwenye hafla ya utoaji wa elimu kwa wananchi huko kisiwani Tumbatu Mkoa wa kaskazini Unguja ,mtuza kumbukumbu wa jumuiya hiyo Ndugu Fikirini Juma Mpwani amesema moja kati ya mambo yanayochukua nafasi ya kuchochea uvunjifu wa Amani wakati wa kuwanadi wagombea ni pamoja upajikaji wa picha za wagombea usiozingatia ridhaa za wamiliki wa maeneo.
Ametaka wananchi kujikita zaidi katika kudumisha amani ili kuweka mazingira ya kufanya ya maendeleo katika jamii zao.Amesema iwapo kutakuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani jamii itatumia muda mwingi kutatua migogoro kuliko kushiriki mambo ya kimaendeleo.

Nae mkufunzi wa jumuiya hioy Bi Amina Hamza Ali amewasihi wananchi kuacha kuandika maneno kwenye karatasi za kura za wagombea ili kuepusha malumbano kwa mawakala wa vyama vya siasa wakati wa kuhesabu kura.
Zoezi la utoaji wa elimu ya mpiga kura kwa wananchi kupitia jumuiya ya muangaza zanzibar limeaza kisiwani pemba na kumalizika kiswani unguja ambapo jumuiya imefika katika mikoa yote ya zanzibar.
